Friday, September 5, 2014

JEURI YA PESA:DOKII AMZAWADIA KIWANJA LUCY KOMBA



Msanii wa filamu na muziki, Ummy Wenceslaus ‘Dokii’ ambaye pesa imemtembelea ameonyesha kuwa na ushoga uliopitiliza na msanii mwenzake Lucy Komba baada ya kumzawadia kiwanja kwenye kicheni pati yake iliyofanyika hivi karibuni.
Msanii wa filamu na muziki, Ummy Wenceslaus ‘Dokii’.
 Dokii akiwa mmoja wa mastaa waliopamba vyema sherehe hiyo iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar, wakati wa kutoa zawadi alisema, yeye na Lucy wametoka mbali na ili kudhihirisha walivyoshibana, anampa kiwanja kilichopo maeneo ya Bagamoyo.
Msanii wa filamu Bongo, Lucy Komba akiwa kwenye kicheni pati yake.
 “Mimi na Lucy tumetoka mbali, tumeshirikiana katika mengi na kudhihirisha upendo wangu kwake namzawadia kiwanja cha eka moja kilichopo Bagamoyo, naamini itakuwa ni kumbukumbu nzuri ya urafiki wetu,” alisema Dokii.