Baba Levo anasema alizitoa hizo taarifa saa tisa mchana sababu ndio aliweza kupata angalau network ya mtandao wa simu kwani kwa saa mbili zilizopita alishindwa kupiga simu baada ya kupata ajali porini kutokana na uzembe wa dereva wa Coaster aliehama upande wake na kuhamia upande wa pili kukwepa barabara mbovu.
Kina Baba Levo walikua kwenye Basi kubwa lililogongana uso kwa uso na Coaster hii ambapo Baba Levo alikua amekaa pale mbele pembeni kabisa ya dereva kwenye kile kigodoro ambapo msanii huyu ilibidi akae hapo sababu kiti chake kiliuzwa ticket kwa watu wawili hivyo aliamua kuiachia siti yake kwa mama wa Kiarabu baada ya kujikuta wote wamepangwa siti moja.
Baada ya ajali hii kutokea, dakika zaidi ya 150 baadae ndio walipata msaada na Baba Levo kwenda Hospitali kucheki afya yake ambapo alisafishwa vidonda alivyoumizwa na vioo vilivyomrukia mwilini kama inavyoonekana kwenye picha za hili basi hapa chini.
Hili ndio Basi walilopata nalo ajali kina Baba Levo ambapo msanii huyu ndio abiria pekee aliejeruhiwa, wengine wote walitoka salama.