Saturday, October 11, 2014

HUYU NDIYE JAMBAZI SUGU LILILOKUWA LIKIWAUA KWA RISASI WANAWAKE JIJINI ARUSHA LAUAWA NA JESHI LA POLISI


Jeshi la Polisi mkoani Arusha limefanikiwa kumuua jambazi aliyekuwa anajihusisha na mauaji ya wanawake mkoani humo ajulikanae kwa jina la Ramadhani Abdallah Jumanne mwenye umri wa miaka 37.

Jamabazi huyo ambaye alikuwa anasakwa kwa muda mrefu aliuawa katika majibizano ya risasi yaliyotokea usiku wa wa kuamkia leo wakati ambao Polisi walifika anapoishi jambazi huyo kwa ajili ya kumkamata.

Taarifa zilizothibitishwa na kamanda mkuu wa Polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas zinaarifu kuwa, Jambazi huyo ametambuliwa na baadhi ya wanawake na alikufa muda mchache alipokuwa anakimbizwa hospitali ya mkoa wa Arusha kwa ajili ya matibabu ili badae afanyiwe upelelezi.

Kabla ya kifo chake Jambazi huyo alikuwa akifanya mauaji hayo kwa kutumia pikipiki ambapo yeye na mwezake ambaye ni dereva walikuwa wanawaua wanawake watembea kwa miguu na baada ya hapo wanachukua baadhi ya viungo kwenye miili ya wanawake hao na kukimbia.

Polisi walimkuta jambazi huyo na risasi pamoja na bastola aina ya SMG na maiti yake iko Makao makuu ya Polisi Arusha.