Sunday, November 23, 2014

MESSI NI MOTO WA KUUSIKIA TU JOTO LAKE, AWEKA REKODI MPYAAAAA BARCA IKUA 5-1

BARCELONA imeibwaga mabao 5-1 Sevilla katika La Liga usiku huu Uwanja wa Camp Nou, huku mshambuliaji Lionel Messi akiweka rekodi mpya.
Muargentina, Messi sasa ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi La Liga kihistoria, 253 akiwa na umri wa miaka 27 tu, akivunja rekodi ya nyota wa zamani wa Athletic Bilbao, Telmo Zarra alifikisha mabao 251 ndani ya miaka 15 kati ya mwaka 1940 na 1955.
Messi amefunga mabao matatu peke yake katika ushindi huo, katika dakika za 21, 72 na 78, wakati mabao mengine ya Barca yamefungwa na Neymar dakika ya 48 na Ivan Rakitic dakika ya 65, huku beki Jordi Alba akijifunga dakika ya 47 kuipatia Sevilla bao la kufutia machozi.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa; Bravo, Alves, Pique, Mathieu, Alba/Adriano dk80, Busquets, Rakitic, Xavi/Rafinha dk77, L Suarez/Pedro dk74, Messi na Neymar.
Sevilla: Beto, Coke, Carrico, Pareja, Diogo, Krychowiak, Banega, D Suarez/Gameiro dk62, Aleix Vidal/Deulofeu dk62, Vitolo na Bacca/Aspas dk74.
Messi (top) is hoisted up high by his Barcelona team-mates after his second goal of the night broke Telmo Zarra's record
Messi (top) is hoisted up high by his Barcelona team-mates after his second goal of the night broke Telmo Zarra's recordMessi (centre) slid home his second - and Barcelona's fourth of the night against Sevilla - to score his 252nd goal in La Liga
Messi (centre) slid home his second - and Barcelona's fourth of the night against Sevilla - to score his 252nd goal in La Liga