MWIGIZAJI Ndumbagwe Misayo maarufu kama Thea, amesema wasanii huvaa sketi fupi ‘vimini’ wakilenga kwenda na wakati na si kujipitisha mbele ya wanaume.
Thea aliiambia Mwanaspoti, kuwa ni kama wanatekeleza wimbo wa mwanamuziki Bwana Misosi ‘Nitoke Vipi’, lakini haimaanishi kwamba wavaaji wote ni wahuni.
“Vimini ni ‘kiki’ tu mjini, watu wengi wanaamini ni sehemu mojawapo ya uvaaji au Nitoke Vipi kama Bwana Misosi alivyosema. Kuna watu wanaamini waigizaji tunaovaa au wanaovaa vimini wanafanya hivyo ili kutafuta biashara, ukweli ni kwamba hakuna kitu kama hicho, kama wapo basi ni kumi kwa mmoja,” alisema Thea.
“Vimini ni ‘kiki’ tu ya mjini. Watu wanaweza kununua filamu kwa sababu wanataka kuona paja la mtu Fulani. Hapo unakuwa umeuza filamu si mwili.”