Wednesday, December 31, 2014

HALI MBAYA YA HEWA YAKWAMISHA ZOEZI LA UOKOAJI MIILI KUTOKA AIRASIA QZ8501

Baadhi ya mabaki ya Ndege ya AirAsia yakiwa Uwanja wa Ndege wa Pangkalan Bun, Indonesia leo.
Mwili wa mmoja wa watu waliokuwa kwenye ndege ya AirAsia ukielea katika Bahari ya Java.
Maofisa wa Kikosi cha Uokoaji wakiichunguza ramani inayoonyesha eneo ilipokutwa miili ya watu waliokuwa katika AirAsia.
Ndugu na jamaa wa watu waliokuwa kwenye Ndege ya AirAsia wakiwa na simanzi baada ya kupata taarifa za kupatikana kwa miili baharini.
JITIHADA za kuopoa miili kutoka katika Ndege ya AirAsia QZ8501 iliyoanguka baharini Jumapili iliyopita ikiwa na watu 162 zimeendelea kukwamishwa na hali mbaya ya hewa.
Ndege hiyo ilianguka katika Bahari ya Java nchini Indonesia na hali ya dhoruba katika eneo la uokoaji imezidi kukwamisha zoezi hilo.
Mamlaka nchini Indonesia yamethibisha kuwa mabaki yaliyoonekana majini eneo la Borneo ni ya ndege iliyopotea ya AirAsia.
Rais wa Indonesia, Joko Widodo, ameahidi kuendelea kufanya uchunguzi wa kina kwa kutumia meli na helkopta kuhakikisha miili ya watu waliokuwa kwenye ndege hiyo inapatikana.
Maombolezo ya pamoja yanatarajiwa kufanyika leo huko Surabaya nchini Indonesia na Gavana wa Jimbo la Java Mashariki, Soekarwo ameeleza kuwa sherehe zote za Mwaka Mpya zimesitishwa kutokana na ajali hiyo ya AirAsia.