Saturday, January 3, 2015

BAADA YA KUMWAGANA:WEMA AUZA GARI LA DIAMOND

Lile gari jipya aina ya Nissan  Murano la staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alilompa aliyekuwa mwandani wake, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ limezua mapya ambapo baada ya kudai linamchefua sasa anadaiwa kuwa analiuza kwa kigezo kwamba hataki gundu mwaka huu mpya wa 2015.
Gari jipya aina ya Nissan  Murano la staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alilompa aliyekuwa mwandani wake, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’
KUMBE LIPO KWA DALALI
Habari za kiwango kutoka kwa mnyetishaji wetu zilidai kwamba gari hilo lipo kwa dalali wa kike maarufu ajulikanaye kwa jina moja la Tindwa kwa ajili ya kulitafutia mteja.
NI KISASI?
Ilidaiwa kwamba, Wema ameamua kufanya hivyo kwa kuwa ana kisasi na hasira kwa Diamond kwa kuwa jamaa huyo kwa sasa anadaiwa kutoka kimapenzi na staa wa Uganda, Zarinah Hassani ‘Zari au The Boss Lady’.
“Watu wanadhani Wema anafurahishwa na Diamond kutupia mapicha na Zari baada ya kuwasifia juzikati.
“Ukweli ni kwamba hivi sasa Wema anakereka sana na jinsi Diamond anavyoweka mapicha yake na Zari wakiwa sehemu mbalimbali na anaona kuwa na gari ambalo  amepewa zawadi na Diamond ni kujipa kero zisizokuwa na sababu hivyo ameamua kuliuza,” kilisema chanzo hicho.
Aliyekuwa mwandani wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
HALIJAPATA MTEJA
Mpashaji wetu huyo alizidi kunyetisha kwamba pamoja na gari hilo kuwa sasa bado liko sokoni lakini halijapatia mteja wa kulinunua kitu ambacho kinazidi kumkera Madam.
“Bado gari halijapata mteja ‘so’ kitendo hicho kinamkera sana  Wema kutokana na gari hilo kutouzika mapema kwa maana kila anapoliona hajisikii vizuri kabisa,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa gazeti kwani ni ‘besti’ mkubwa wa Wema.
WEMA ANASEMAJE?
Baada ya kupewa ubuyu huo, gazeti hili lilimsaka Wema ambaye alipopatikana alidai yupo bize akiandaa shoo zake za mkoani Dodoma na Morogoro.
“Ngojeni kwanza nimalize shoo zangu za mikoani. Kwa sasa nipo Dodoma nikimaliza naenda Morogoro,” alisema Wema kwa ahadi kuwa atafafanua suala hilo vizuri akitulia.
‘Diamond Platnumz’ akiwa na aliyekuwa mwandani wake Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
TUMEFIKAJE HAPA
Diamond alimzawadia Wema gari hilo lenye thamani ya Sh. milioni 36,  siku ya bethidei ya mwanadada huyo iliyofanyika Septemba 28, mwaka jana.
Siku chache baadaye Wema alidai kummwaga jamaa huyo huku akieleza kwamba hapendi kuliona wala kulitumia gari hilo kwani lilikuwa likimzidishia chuki juu ya jamaa huyo.