WAZIRI wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu ambaye ametangaza nia ya kuwania urais wa nchi amefanya kufuru kubwa katika Kanisa la Efatha linaloongozwa na Nabii Josephat Mwingira, mjini Kibaha, Pwani baada ya kusakata sebene la Injili usiku wa manane.
Nyalandu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini (CCM), alifanya hayo juzi katika mkesha wa kuukaribisha mwaka mpya 2015 ambapo alipanda jukwaani na kusakata muziki huku akishangiliwa na waumini wa kanisa hilo.
Kuonesha msisitizo, Nabii Mwingira naye aliingilia jukwaani na kucheza muziki huo wa Injili huku akighani maneno ya Mungu kwa kutumia kipaza sauti alichokuwa nacho mkononi saa zote za hafla hiyo.
Mara baada ya saa sita na dakika 35 usiku kutimia Nyalandu ambaye alikuwa mgeni rasmi alikaribishwa kusema neno ambapo alipanda jukwaani na kumshukuru Mungu kwa kuuona mwaka mpya 2015.
Hata hivyo, alijipigia kampeni kwa kuwakumbusha waumini hao kuwa Oktoba mwaka huu Tanzania itakuwa na tukio kubwa, hivyo waumini hao kwake ni muhimu kwani wakati ukifika atawaomba kura zao.
“Wakati nacheza pale nimewaona wanakwaya na kuhisi kwamba wana kitu moyoni. Nawaambia Oktoba ikifika lazima mchague vijana nami nitawahitaji sana kuja kuniimbia,” alisema.
“Wakati nacheza pale nimewaona wanakwaya na kuhisi kwamba wana kitu moyoni. Nawaambia Oktoba ikifika lazima mchague vijana nami nitawahitaji sana kuja kuniimbia,” alisema.
Naye Nabii Mwingira alisema mwaka 2015 anatamka wale wote ambao wapo kanisani hapo na wana dhamira moyoni mwao, watatimiziwa na Mungu wa Efatha.
“Huwa sisi hatuamini katika mashetani, tunaamini katika roho saba... hivyo natamka kwamba wote waliopo hapa na wana nia zao katika vifua vyao, basi Mungu atawapa,” alisema Mwingira huku akishangiliwa.
Hii ni mara ya pili kwa Nyalandu kujipigia kampeni za urais kanisani, mara ya kwanza ni hivi karibuni katika jimbo lake alipokwenda katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kijijini Ilongelo, Singida.
Kiongozi huyo pia alikwenda katika Shule ya Msikiti wa Ilongelo ambapo inadaiwa alitoa msaada wa kusaidia shule na kanisa hilo.
Kiongozi huyo pia alikwenda katika Shule ya Msikiti wa Ilongelo ambapo inadaiwa alitoa msaada wa kusaidia shule na kanisa hilo.
Hata hivyo, baadhi ya wadau wa siasa waliozungumza na gazeti hili juzi jijini Dar walisema kuwa anachofanya Nyalandu ni kinyume na maadili ya chama chake ambacho kinakataza kutumia makanisa na misikiti kujipigia debe katika mambo ya siasa.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Taifa wa CCM, Nape Nnauye hakupatikana ili aweze kutoa maoni yake kuhusu vitendo hivyo kwani simu yake ilikuwa haipatikani.
Baadhi ya wagombea waliotangaza nia kutoka CCM ni Dk Hamisi Kigwangalla, Januari Makamba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na wengine wanaotajwatajwa ni Steven Wassira, Bernard Membe, Samwel Sitta na Edward Lowassa.