Saturday, January 3, 2015

JOKATE: SIPENDI ‘SINI’ ZA KUTOMASWA!

Mwanamitindo ambaye pia ni msanii wa filamu Bongo, Jokate Mwegelo.
Stori: Laurent Samatta
MWANAMITINDO ambaye pia ni msanii wa filamu Bongo, Jokate Mwegelo amesema kuwa hapendi kuigiza sini za mapenzi hasa zile anazotakiwa kushikwashikwa na mwanaume hasa asiyemjua.
Jokate alifunguka hayo wakati paparazi wetu alipotaka kujua namna ambavyo wazazi na mpenzi wake wanavyolipokea suala la yeye kuigiza sini za kushikwashikwa na wanaume tofauti katika filamu ndipo alipofunguka kuwa suala hilo limekuwa likipigwa vita na wazazi wake lakini analazimika kufanya kwa sababu ndiyo kazi aliyoichagua.
Jokate Mwegelo akipozi.
“Wazazi wangu wanachukia sana jambo hili na huwa wanasema bora niache filamu, hata mimi mwenyewe huwa sipendi ila huwa navumilia kwa kuwa ni kazi, sina jinsi,” alisema Jokate.