Kaa chonjo! Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), mheshimiwa Kassim Majaliwa amejikuta akitumbukia kwenye kamera za Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers baada ya kuchunguzwa kwa kuingia hotelini akiwa ametanguliwa na mrembo mmoja aliyedaiwa kuwa na ahadi naye, Ijumaa Wikienda lina picha kamili.
Gari la mheshimiwa Kassim Majaliwa likiwa eneo la tukio.
OFM ilimshughulikia waziri huyo juzikati kwenye hoteli ya kisasa ya nyota tatu iliyopo maeneo ya Bamaga-Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo mheshimiwa huyo aliingia.HABARI KAMILI
Majira ya saa 11:05 jioni OFM ilipata taarifa kutoka kwa chanzo chetu kilichopiga simu na kueleza kuwa Waziri Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Dodoma ameingia hotelini hapo akiwa ametanguliwa na mrembo huyo.
Mpambe wa mheshimiwa Kassim Majaliwa akilikagua gari hilo.
“Mimi ni msomaji wenu. Niko hapa hoteli ya....(anaitaja jina). Yule waziri wa JK, anayeitwa Kassim Majaliwa amekuja na gari aina ya Toyota Harrier nyeupe, ameshuka na kuingia hotelini. Lakini dakika kumi kabla kuna mrembo mkali ameingia hapa huku anazungumza na simu, nahisi wana ahadi naye,” kilisema chanzo chetu.SAA 11:10, OFM YATUA HOTELINI
Kikosi kazi cha OFM kilijikusanya na kuingia ndani ya gari kisha yakakanyagwa mafuta hadi kwenye hoteli hiyo ambapo kilishuhudia gari la mheshimiwa huyo likiwa limeegeshwa.
...Akiendelea kulikagua kabla ya kuondoka hotelini hapo.
OFM SAMBAMBA NA GARIIli kumtega vyema, OFM waliegesha gari lao kwa kupeana mgongo na la waziri na kusubiri kwa muda huku macho ya kamera yakiangalia kwenye mlango mkubwa wa kuingilia hotelini hapo na wakati mwingine kwenye gari la mheshimiwa.
SAA 11: 22, OFM NDANI YA HOTELI
Baada ya kuona muda unakwenda, mmoja wa watenda kazi wa OFM alitoka kwenye gari na kuzama ndani ambapo alipanda mpaka ghorofani kwa lengo la kuchunguza chochote.
OFM ilibahatika kukutana na mhudumu mmoja ambaye alisema hajamuona mheshimiwa huyo, akamshauri kwenda kujaribu kumuangalia upande wa baa, jambo ambalo kachero huyo wa OFM alilifanya.
Mheshimiwa Kassim Majaliwa akipanda kwenye gari hilo.
SAA 11: 26, OFM, WAZIRI MACHO KWA MACHOKachero wa OFM alitembea hadi kwenye baa ya hoteli hiyo na kukutana na mheshimiwa ana kwa ana (lakini hawafahamiani).Waziri huyo alikuwa amekaa na wanaume wengine wanne wakizungumza. Mazungumzo yao yaliashiria yana msisitizo kama si umuhimu kwa wote.
SAA 11: 30, OFM ARUDI KUTEGA GARINI
Hata hivyo, OFM hakukubaliana na kumkuta mheshimiwa huyo amekaa na wanaume wenzake, alirudi ndani ya gari na kuwapa taarifa wenzake ambao katika kujiongeza walikubaliana kutulia ndani ya gari hadi kuona mwisho wake.
JUA LAANZA KUPOTEZA NURU
Saa 11: 43, jua lilianza kupoteza nuru yake kuashiria kwamba, mchana unakatika na giza linakaribia kupiga hodi.
WAZIRI HUYOOO!
Ilikuwa saa 11:47, ghafla Waziri Majaliwa alitoka hotelini hapo akiwa ameongozana na mwanaume mmoja ambaye OFM hawakuweza kumjua ni nani!
Ilikuwa saa 11:47, ghafla Waziri Majaliwa alitoka hotelini hapo akiwa ameongozana na mwanaume mmoja ambaye OFM hawakuweza kumjua ni nani!
Mheshimiwa Kassim Majaliwa akiwa kazini.
Mheshimiwa huyo alikwenda upande wa dereva lakini kabla hajaingia, mwenzake alilizunguka gari na kuinama kuchungulia chini kukagua usalama. Baada ya kujiridhisha, waliingia wote ndani ya gari na kuondoka zao.ALISTAHILI KUJIENDESHA?
Baada ya mheshimiwa kuondoka, OFM walijiuliza kama ni halali kwa waziri kujiendesha mwenyewe badala ya dereva ambaye kila waziri hupewa na serikali.
Ili kutaka kujua hilo, OFM walimtwangia simu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi, mheshimiwa Hawa Ghasia na kumuuliza kama ni sahihi kwa waziri kuendesha gari mwenyewe.
“Kama waziri ana safari zake binafsi na si muda wa kazi hakuna shida. Hata kama ni muda wa kazi anaweza kujiendesha mwenyewe lakini kwa gari binafsi siyo la serikali,” alisema mheshimiwa Ghasia.
PONGEZI WAZIRI MAJALIWA
OFM imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kufichua maovu katika jamii ya Tanzania. Hivyo, kama kweli Waziri Majaliwa agekuwa ameingia na kimwana kwenye hoteli hiyo lazima OFM wangemnasa tu. Lakini alionesha mkubwa. Kwa sababu hiyo, Ijumaa Wikienda linammwagia pongezi kibao.