Mshambuliaji machachari wa timu ya soka ya
Simba, Emmanuel Okwi, jana jioni
amenusurika kifo baada ya kupigwa kiwiko
nyuma ya kichwa kwenye mishipa ya fahamu
na kuzimia kwa dakika kadhaa uwanjani.
Mkasa huo ambao umethibitishwa na daktari
wa timu hiyo, Yassin Gembe, ulitokea wakati
wa pambano la ligi kuu ya Vodacom baina ya
timu hiyo na Azam FC lililopigwa kwenye
uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuisha kwa
sare ya bao 1-1. Bao la Simba lilifunwa na
Okwi wakati lile la Azam likiwekwa kimiani na
Kipre Tchetche.
Kwa mujibu wa Gembe, Okwi alipatiwa huduma
ya kwanza uwanjani hapo kabla ya kupelekwa
kwenye zahanati iliyoko pia uwanjani hapo na
kisha baadaye kukimbizwa Hospitali ya Rufaa
ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
“Ilikuwa mbaya sana na angeweza hata
kupoteza maisha,” alisema Gembe na
kuongeza;
“Tuliendelea kumpatia matibabu kwenye zahati
ndogo uwanjani hapo mpaka aliporejesha
fahamu ndipo tukaanza kuelekea Muhimbili
kwa matibabu zaidi yaliyochukua takribani
masaa mawili. Ila kwa sasa yuko vizuri.”
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa za daktari,
Okwi atakuwa nje ya uwanja kwa siku kadhaa
wakati akiwa chini ya uchunguzi kuangalia
maendeleo ya afya yake. Hiyo ni pamoja na
kuwa nje katika ratiba ya mazoezi ya timu
hiy