Sunday, February 22, 2015

JACK WA CHUZ AFUNGUKA HAYA BAADA YA KUVUNJIKA KWA NDOA YAKE

 

Jack alisema, kwa muda aliodumu kwenye ndoa ameshaona raha na karaha yake hivyo suala la kuolewa tena sasa hivi halipo akilini mwake.

“Katika ndoa lazima kuwe na mabaya na mazuri, hata hivyo siwezi kusema ndoa ni chungu hapana, ila mimi kwa sasa hivi nimeona nipumzike kwanza sitaki tena ndoa labda kwa hapo baadaye nitakapojipanga tena upya,” alisema Jack.

Jack alidumu na mumewe huyo kwa miaka miwili na nusu kabla ya kupewa talaka hivi karibuni huku chanzo kikiwa ni kusalitiana katika mapenzi.