Thursday, February 12, 2015

MAMA LULU AMEIBUKA NA KUMKATAA ALIYETAKA KUMUOA LULU


Kufuatia kauli yake ya hivi karibuni kuwa nyumba anayomiliki ilitokana na mchango wa bwana’ke (hakumtaja jina), mama mzazi wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila ameibuka na kumkataa mwanaume huyo.


Mama mzazi wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila.

Kwa mujibu wa Lulu, nyumba hiyo iliyopo Kimara jijini Dar ameijenga kwa kusaidiana na bwana’ke kwa mtindo wa pasu kwa pasu (kuchangia nusu kwa nusu).Alisema kuwa anamshukuru Mungu kwani hadi hapo ilipofikia ikiwa inakaribia kumalizika ameijenga kwa nguvu zake na mwanaume wake huyo.


“Yeah! Nimejenga kwa msaada wa mwanaume wangu, tunasaidiana nusu kwa nusu,” alinukuliwa Lulu.
Pamoja na mbwembwe zote hizo za staa huyo kwa jamaa yake huyo, mama mzazi wa Lulu ameliambia Amani kwamba hamtambui mwanaume huyo kwani hajawahi kwenda kujitambulisha kwake pamoja na kwamba kahusika kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo.

Alifunguka: “Sijawahi kutambulishwa na Lulu kama ana mchumba.
“Kwa hiyo awe amemsaidia au hajamsaidia, mimi simtambui.
“Ingekuwa Lulu amewahi kumtambulisha kwangu kuwa huyo ndiye mchumba wake hapo sawa lakini hakuna kitu kama hicho.


“Halafu naomba utambue kwamba Lulu hawezi kumtambulisha bwana’ke au boy friend wake kwangu, siyo heshima labda awe mchumba. Hapo kidogo afadhali lakini mtu tu mtu, hakuna kitu kama hicho.
Kabla ya Lulu kueleza ukweli juu ya ujenzi wa nyumba hiyo, awali kulikuwa na madai kwamba alihongwa na mheshimiwa mmoja (jina tunalo) huku wote wakikanusha kwa nyakati tofauti.

Hata hivyo, kitendo cha Lulu kumiliki mjengo huo kimempa heshima kubwa tofauti na mastaa wenzake wa kike ambao wamekuwa wakiishia kupangiwa nyumba na kuhongwa magari yasiyo na kadi kisha kunyang’anywa na kurudia maisha ya kawaida uswahilini.