Friday, February 6, 2015

MAMA MZAZI WA NAY WA MITEGO ANAHISI MWANAE NI FREEMASON NA HATAKI KUPOKEA FEDHA YAKE

Mama mzazi wa Nay wa Mitego anahisi
mwanae ni mfuasi wa jamii ya siri ya
freemason na ameanza kusita kupokea
fedha kutoka kwake.
Kwa mujibu wa mama yake, mafanikio ya
haraka ya Nay yakiwemo kujenga nyumba
ya kifahari, kumiliki magari kadhaa na
maisha yake ya kimilionea, vimemfanya
aamini maneno yanayosemwa na watu au
kuandikwa kwenye magazeti ya udaku
kuwa mwanae amepata utajiri huo kwa
njia isiyo halali.
“Kuna kipindi ambapo nimetoa wimbo
wa Mr Nay baada ya kutoka ile video
nakumbuka mimi mama yangu huwa
nampelekeaga hela ya matumizi kila
baada ya wiki mbili au mwezi mmoja.
Kuna kipindi nilimpelekea hela akasema
‘no’ mbona mimi hela bado ninayo,” Nay
alikiambia kipindi cha Amplifaya cha
Clouds FM.
Nay anasema alimpelekea mama yake
kiasi cha shilingi laki mbili ama tatu na
akagundua kuwa mama yake hasemi
ukweli na kuna kitu kilikuwa
kikimsumbua akilini.
“Baada ya hapo akaniambia ‘kuna habari
nasikia kuhusu huu wimbo wako huu
nimeona mambo ya ajabu ajabu mule
nimeona magazeti majirani wamekuja
wameniambia hivi na hivi’,” aliongeza
Nay.
“Halafu bahati nzuri nilikuwa nimetoka
kununua hii gari yangu ambayo
natembelea sasa hivi ‘Morano’
alivyoniuliza hivyo nikaona mama yangu
hataki hela yangu sababu ana wasiwasi na
hiki ambacho watu wanaongea. Hilo ni
tatizo lililonipa wasiwasi na moyo wangu
ukaingia unyonge, for real kabisa nikawa
mpole.”
“Lakini nikawa na imani kwamba endapo
mama yangu angekuwa anatambua
kwamba huu muziki ungekuja kuniweka
sehemu uflani tangu zamani angekuwa
ananisupport zile hustle mazingira
magumu niliyokuwa napitia angekuwa
anajua basi sasa hivi ningekuwa naenda
naye sawa.”
Nay amesisitiza kuwa mali anazopata ni
neema za Mungu tu.
“Mwenyezi Mungu tu ameamua
kuninyooshea kuniwekea mambo yangu
sawa japokuwa bado sijafika pale
ninapotaka kufika,” alisisitiza rapper
huyo.