Sunday, April 12, 2015

Diamond Platnumz: Mbunge Halima Mdee ni Mzigo Jimbo la Kawe

Msanii maarufu nchini mwenye mafanikio makubwa katika sanaa ya mziki wa kizazi kipya, Diamond Platnumz, amevunja ukimya wake juu ya ubovu wa barabara iendayo Madale ambayo ipo kwenye jimbo la Kawe chini ya Halima Mdee.

Msanii huyo ameelekeza lawama zake kwa mbunge huyo wa kupitia tiketi ya CHADEMA kwa kuwa Halima Mdee aliahidi wananchi wa jimbo hilo kuwa katika kipindi chake cha ubunge atahakikisha barabara hiyo inajengwa kwa kiwango cha lami, lakini hadi hii leo barabara imejaa tope tu!

Diamond alieleza masikitiko yake huyo kupitia katika kituo cha Clouds TV pale alipoulizwa swali kuhusu makazi yake mapya yaliyopo katika jimbo la Kawe na ndipo hapo akafunguka kuhusu suala hilo la kero ya barabara ambalo lina muda mrefu alijashughulikiwa na mbunge Halima Mdee.