Monday, May 25, 2015

BASI LACHOMWA MOTO NA WAANDAMANAJI MJINI BUJUMBURA, BURUNDI

Vurugu za kuchoma moto vitu mbalimbali zikiendelea.
Waandamanaji wakiendeleza maandamano mjini Bujumbura.
Magurudumu yakichomwa moto, barabara ikiwa imefungwa na waandamanaji.
Bujumbura, Burundi
Basi moja la abiria limechomwa moto mjini Bujumbura, Burundi na waandamanaji wanaopinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kuwania urais muhula wa tatu kinyume na katiba ya nchi hiyo.
Tukio hilo limetokea mapema leo katika Kitongoji kimoja kilichopo eneo la Kanyosha mjini Bujumbura ambapo waandamanaji wamechoma basi hilo na magurudumu ya magari barabarani huku Polisi nao wakirusha risasi kuwatawanya waandamanaji hao.
Kwa takribani wiki kadhaa sasa, kitongoji hicho kimekuwa kitovu cha maandamano haya dhidi ya awamu ya tatu ya rais Nkurunziza.
Maandamano haya yanarejea upya baada ya kuuawa kwa kiongozi wa Chama cha upinzani, Zedi Feruzi nje ya nyumba yake katika mjini Bujumbura.
Aidha wanaharakati wa upinzani nchini humo wamesitisha mazungumzo na serikali ya rais Pierre Nkurunziza ya kutaka kutanzua mzozo huo wa kisiasa.
Uamuzi ambao wengi wanasema kuwa unaenda kinyume na sheria na ndio iliyosababisha kuwepo kwa jaribio la kumpindua, na maandamano ya wiki kadhaa.
Tayari zaidi ya raia 100,000 wa taifa hilo wamekimbia mapigano nchini humo na kwenda nchi jirani za Rwanda na Tanzania.
NA BBC