Kile kipindi bora kabisaa cha burudani ambacho kilikuwa kikiruka kila siku ya Jumamosi kuanzia saa Nne kamili asubuhi mpka saa sita mchana, Jumamosi hii kinafikia tamati na hakitosikika tena Jumamosi, akipiga stori na Power Jams ya East Africa Radio
wa kipindi hicho Dullah alimaarufu kama Mjukuu amesema kuwa yeye amekua mtangazaji wa kipindi hicho huu mwaka wa saba lakini anasikitika kuachana na kipindi hicho, sababu anatambua kuwa vijana wengi walikuwa wakikifuatilia na kukisikiliza ila hana namna zaidi ya kuwaaga.
"Jumamosi hii Planet Bongo itakuwa ndiyo show ya mwisho kabisaa, Mjukuu wa Ambua ni mwaka wa saba sasa nimekuwa nikiishi nayo hiyo show naamini kabisaa ni stori mbaya hizi sababu mashabiki waliipenda na kila Jumamosi ni show iliyokuwa ikisikilizwa sana asubuhi. Nachoomba mashabiki wangu wasikilize Show ya mwisho wa Planet bongo ili tuagane vizuri hivyo kuna vitu fulani vizuri kama Suprise ambavyo vitakuwepo siku hiyo."
EATV