- Nafasi tatu za juu zimechukuliwa na Johannesburg, Casablanca na Durban
- Ripoti ya YouthfulCities imetolewa kuyahusu majiji hamsini na tano duniani baada ya utafiti uliotumia viashiria 101
London, 7 Mei 2015: DAR ES SALAAM leo imetajwa kuwa jiji bora la 6 kwa vijana Afrika na jiji la 53 katika majiji bora kwa vijana duniani kulingana na utafiti mkubwa na wa aina yake uliofanyika katika majiji yote makubwa duniani na uliozingatia mtazamo wa vijana.
Dar es salaam ilifanya vizuri katika maeneo mbalimbali ikiwemo sanaa na ujasiriamali.
Johannesburg imeishinda Casablanca na kushika nafasi ya kwanza katika kanda ya Afrika.
Casablanca imechukua nafasi ya pili na imefanya vizuri katika usalama na mazingira.
Moja ya lengo kubwa la mradi huu ni kutoa changamoto kwa vijana kubadili majiji yao.
Kwa mwaka 2015 ripoti ya YouthfulCities imetoka kwa majiji 55 duniani kote kwa kupitia viashiri 101 kama vile usafiri, ajira na michezo.
Mpango huu ni jaribio la kwanza kuangalia ni majiji gani yanafaa sana kwa vijana wenye miaka 15-29. Mpango huu pia unatoa mwangaza wa majiji yanayokuwa kwa kasi.
Vijana wana nafasi muhimu sana katika miji mikubwa. Karibu kila kanda duniani imeingiza jiji katika nafasi ishirini za juu.
Amerika ya kaskazini- Majiji 9; Ulaya - Majiji 5; Asia - Majiji 3 huku Tokyo ikiwa katika nafasi ya kwanza na ya 12 duniani, America kusini- Majiji 2 na jiji la Mexico City likiongoza na likiwa katika nafasi ya 9 duniani.
Mashariki ya kati Tel Aviv imeshika nafasi ya 14 duniani. Jiji lililoongoza Africa ni Johannesburg likiwa katika nafasi ya 35 duniani. Kanda zote duniani zina majiji katika nafasi 25 za mwisho.
Sonja Miokovic, ambaye ni Mwanzilishi wa YouthfulCities alisema:‘’Tuko katika wakati ambapo tuna nafasi ya kubadili sehemu tunazoishi, sehemu tunazofanya kazi na sehemu tunazocheza kwa kushikirisha rasimali kubwa ambayo bado haijatumika, ambayo ni Vijana!
"Nusu ya watu wote duniani wako chini ya miaka 30 na nusu kati yao wanaishi katika miji mikubwa duniani.
"Vijana na miji haswa mikubwa watabadilisha dunia huko mbeleni. Ndiyo maana ni muhimu kwa miji mikubwa kuwashirikisha vijana na kutafuta njia ya vijana kuonyesha uwezo wao.’’
Francis Kessy na Joachim Mangilima, wawakilishi wa YouthfulCities katika jiji la Dar es salaam wanasema:
‘’Ukitembea mitaani katika jiji la Dar es salaam utaona vizuri jinsi ambavyo vijana ni wengi katika jiji la Dare s salaam. Ripoti ya YouthfulCities inaonyesha wapi Jiji linahitaji kuwekeza katika kuboresha hali ya maisha ya vijana ikiwemo katika Afya na Elimu."