Thursday, May 28, 2015

YULE MME WA IRENE UWOYA AIBUKA NA HAYA MAPYA KUMBE HAWAJAACHANA

Mume wa Staa wa filamu za Kibongo,Irene
Uwoya, Hamad Ndikumana ‘Katauti’amesema
kuwa hajaachana na msanii huyo kama
ambavyo baadhi ya watu wanavyodhani.
Ndukumana ambaye ni mwanasoka kwenye
klabu moja ya soka nchini Rwanda
ameyazungumza hayo hivi karibuni wakati
alipofanya mahojiano na mtangazaji wa Clouds
TV,Zamaradi Mketema alisema kuwa ingawa
hawaishi pamoja na Irene Uwoya lakini
hawajaachana.
‘Sijaachana na Irene Uwoya ingawa hatuishi
pamoja yeye anaishi Dar mie naishi Rwanda na
bado nacheza soka ila nategemea kusomea
ukocha baada ya kustaafu soka ,’alisema
Ndikumana.
Irene na Ndikumana walifunga ndoa mwaka
2008 na kubahatika kupata mtoto mmoja
aitwaye Krish.
Cloudsfm.com