Ishu hiyo ilijiri wikiendi iliyopita maeneo ya Mtaa wa Kongo-Kariakoo jijini Dar ndani ya basi la UDA ambapo kijana huyo alidaiwa kukwapua simu hiyo.
Akiwa chini ya ulinzi baada ya kukwapua simu.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, shuhuda wa tukio hilo alisema: “Kiukweli jamaa alipigwa sana, kama siyo polisi kunusuru uhai wake angeuawa na wananchi waliokuwa na hasira,’’ alisema shuhuda na kuongeza kuwa polisi waliokuwa doria waliondoka naye kwenda kituo cha polisi ili sheria ichukue mkondo wake.