Nature akiweka maiki vizuri ili akamue ipasavyo.
Profesa J akiwapa mashabiki kitu walichotaka.
SHOO ya kutimiza kutimiza miaka 16 katika muziki kwa msanii Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’ na kituo cha Utangazaji cha EFM kutimiza mwaka mmoja iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Burudani wa Taifa wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, lilikuwa moto wa kuotea mbali.
Katika onyesho hilo Nature, mbali ya kutoa burudani ya nguvu, alipigwa tafu na Snura, Profesa J. Makomandoo, Shetta na Msaga Sumu.