Tuesday, September 15, 2015

Mbaroni kwa kutesa mahausigeli

AMTESA HOUSE GIRL (2)Anna Livingstone Mushi akipandishwa kwenye gari la polisi tayari kupelekwa kituoni
Na Joseph Ngilisho Arusha
Mwanamke mmoja, Anna Livingstone Mushi (38),  mkazi wa Oldadai wilayani Arumeru, ametiwa mbaroni na polisi kwa madai ya kuwapiga mijeledi ya waya wa umeme, kuwachoma na pasi mgongoni na kuwakata makalio mahausigeli wake wawili.
Wasichana  hao Rehema Musa (20),  mkazi wa Singida na mwenzake, Jesca Mathiasi (15), mkazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru wakipatiwa matibabu kutokana na majeraha makubwa sehemu za mwilini mwao.
AMTESA HOUSE GIRL (1)…Akiwa kwenye gari la polisi.
Akizungumza kwa tabu, Rehema ambaye amejeruhiwa vibaya mgongoni na kukatwa makalio alisema kuwa aliajiriwa kufanya kazi za ndani na mama huyo tangu mwaka jana akitokea mkoani Singida .
Alisema akiwa na mwenzake, tajiri yao Anna ambaye ni maarufu kwa jina la mama Malaika aliwafundisha kutengeneza keki kama biashara yake anayoifanyia nyumbani kwake.
Alidai kuwa tajiri huyo alikuwa akiwapiga bila sababu za msingi, kuwanyima chakula na kuwafungia kwenye mabanda ya kuku hadi wapone majeraha na kuwazuia  kutoka nje ya uzio wake au kutoa taarifa  kwa mtu yeyote huku akiwatishia kuwaua na kuwazika katika eneo lake wakitoa siri.
Alidai kuwa siku ya tukio Septembe, 7 mwaka huu tajiri yao alikuta baadhi ya keki zimeungua ndipo alipoanza kuwachapa kwa waya za umemei baada ya kuwavua nguo zote na kama aitoshi aliwaunguza kwa pasi iliyokuwa na moto na baadae alichukua kisu na kuwakata makalio.
Alieleza kuwa wakati wakipigwa mwenzake Jesca alifanikiwa kutoroka kwa kuruka ukuta ambapo alianguka na kupoteza fahamu na alipozinduka alitoa taarifa kwa mmoja wa majirani wa eneo hilo ambaye pia aliiarifu uongozi wa serikali ya mtaa wa eneo hilo nao ukawataarifu polisi.
Alisema mara baada ya jeshi la polisi kufika eneo la tukio mtuhumiwa aligoma kufungua mlango ndipo polisi hao walipo amua kuruka ukuta na kufunja kufuli na kumkamata mtuhumiwa.
Hata hivyo, mtuhumiwa huyo aligoma kuwaonyesha msichana mwingine aliyemkata makalio ambaye alimficha katika kabati la nguo ili asionekane kwa lengo la kupoteza ushahidi.
Naye mwenyekiti wa kijiji hicho cha Olidadai, Lazaro Mollel alisema tukio hilo  ni lakinyama na kwamba haikuwa rahisi lwao kugundua kutokana na mtuhumiwa kutotaka mtu yeyote kuingia katika nyumba yake wala mfanyakazi kwake kutoka nje.
Aliongeza kuwa yeye kama Mwenyekiti wa kijiji alipata taarifa baada ya moja ya wasichana wake kufanikiwa kutoroka wakati wakipigwa.
Jeshi la polisi mkoani arusha limethibitisha kutokea kwa tukio hilo afisa mmoja wa upelelezi aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa siyo msemaji alisema mtuhumiwa anashikiliwa baada ya kufunguliwa jalada la mashitaka lenye kumbu kumbu namba AR/RB/11455/2015 na atavikishwa mahakamani mara baada ya upelekezi kukamilika.