Brighton Masalu
STAA wa filamu Bongo, Irene Paul ‘Smart Girl’ amezua mshangao baada ya kupiga mayowe huku akirusha mikono kushangilia tuzo aliyopata jambo lililozua miguno kwa waliomshuhudia.
STAA wa filamu Bongo, Irene Paul ‘Smart Girl’ amezua mshangao baada ya kupiga mayowe huku akirusha mikono kushangilia tuzo aliyopata jambo lililozua miguno kwa waliomshuhudia.
‘Katukio’ hako ‘amazing’ kalishuhudiwa na paparazi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Jengo la Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar kulikokuwa na sherehe ya utoaji Tuzo za TAFA na kuwafanya baadhi ya watu kuacha kila kitu kwa muda na kumtumbulia macho.
Msanii huyo alipata tuzo hiyo kwa kipengele cha The Best Actress (Supporting Role) kupitia Filamu ya Never Give Up aliyoshirikiana na msanii kutoka Nigeria, Joseph Van Vicker na kuonekana kuchanganyikiwa namna hiyo.
Baada ya kuchukua tuzo hiyo, ‘kiruka njia’ wetu alimfuata na kumuuliza kulikoni aonekane kupagawa kwa kiwango hicho ambapo alisema kutokana na ugumu wa kipengele hicho kwani alikuwa akichuana na watu anaowaheshimu sana katika tasnia ya filamu, alioamini wana kiwango cha juu kuliko yeye hivyo hakuamini kilichokuwa kinatokea kwa wakati huo.