Saturday, May 30, 2015

WEMA, IDRIS NUSU WAZICHAPE KISA .....

Musa mateja
MALKIA anayemiliki Kampuni ya Endless Fame Production, Wema Isaac Sepetu na Mshindi wa Big Brother Africa 2014/15, Idris Sultan ambao wamekuwa marafiki wakubwa katika siku za hivi karibuni, nusu wazichape kavukavu baada ya kupishana kauli huku wivu wa kimapenzi ukitajwa.
Malkia anayemiliki Kampuni ya Endless Fame Production, Wema Isaac Sepetu.
Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita nje ya Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro iliyopo Posta jijini Dar ambapo kwa pamoja walikuwa wamehudhuria sherehe ya utoaji Tuzo za Watu.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tafrani ya wawili hao kutaka kukunjana ilitokea baada ya kumalizika kwa shuguli hiyo ambapo Idris alimpora Wema tuzo yake aliyoshinda na kwenda nayo kwenye gari lake.
Ugomvi huo ulipamba moto na kusababisha watu waliokuwa wakiwashuhudia kutaharuki ambapo Wema alikwenda kwenye gari lake lililokuwa likiendeshwa na Petit Man lakini Idris alimfuata akionekana kumuonea wivu na kumtaka apande gari lake waondoka jambo ambalo Wema alilitolea nje na kumfungia kioo.
Mshindi wa Big Brother Africa 2014/15, Idris Sultan.
Baada ya kuona Wema amemtolea nje, Idris alikwenda kwenye gari lake na kuliegesha mbele ya gari la Wema ‘kum-block’ ili asiondoke ambapo alishuka na kumwambia Petit Man ahakikishe anamfuata kwa nyuma jambo ambalo Petit Man alishindwa kulitekeleza baada ya Wema kukataa.
Baada ya kushuhudia vurugu hizo, mwanahabari wetu alimfuata Wema ili kujua kilichotokea ambapo mwanadada huyo alisema kuwa haelewi ni kitu gani ambacho kilimkuta Idris siku hiyo maana kama angekuwa anakunywa pombe, angesema labda alizidiwa lakini kwa kilichotokea hadi leo hajui ni kipi kilimkuta.
Wema Isaac Sepetu akiwa na Idris Sultan.
“Yaani hata sielewi Idris alifikwa na nini maana amefanya mambo ya ajabu sana na mara ya kwanza nilijua utani lakini nilimshangaa zaidi baada ya kukomaa hadi kufikia hatua ya kuni-block na gari lake huku akitaka niondoke naye wakati kila mtu alikwenda pale kimpango wake.“Mimi nadhani kuna utoto fulani bado anao na unamsumbua,” alisema Wema lakini Idris hakupatikana kusema chochote.