Friday, July 10, 2015

Picha 11 za kituo cha Polisi kilichochomwa moto leo Dar

.
.
Taarifa ninayokusogezea ni hii kuhusu kituo cha polisi  eneo la ‘Bunju A’ Dar es Salaam kilichochomwa moto na wananchi baada ya tukio la ajali ya gari kumgonga mtoto mmoja.
.
.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura ‘Hapa kituo kimechomwa moto lakini kabla ya uchomwaji wa kituo hiki kulikuwa majira ya asubuhi kati ya saa moja na nusu kulikuwa na tukio la ajali lililosababisha kifo hapa maeneo ya Bunju A majira hayo gari moja aina ya Coast ilikuwa ikitoka Bagamoyo na kusababisha kumgonga mwanafunzi Thabisa Omary mwenye umri wa miaka 11 anasoma Bunju A darasa la nne n ilisababisha kifo chache’ – Camillius Wambura (RPC)
.
.
‘Kwahiyo kutokea kwa ajili hiyo wanafunzi waliweza kuingia Barabara wakaziba barabara zote kuanzia Bunju A mpaka Bunju B wakilalamika kwamba awali kulikuwa na Matuta lakini matuta na sasa magari yanapita kwa mwendo kasi na kusababisha vifo lakini walitoa matamko kwamba wanataka watu wenye mamlaka na Barabara wafike na kuweka matuta kama yalivyokuwa ili yaweze kupunguza Ajali na vifo’ – Camillius Wambura (RPC)
.
.
‘Sasa baada ya sisi Polisi kufika na kusikia tamko hilo tuliwasiliana na mamlaka ya Tan Road walituma watu kuja kuwasikiliza wanafunzi wale lakini kuona maeneo ambayo yanalalamikiwa kwamba yalikuwa na matuta na hayana basi nakujua ni hatua gani wanaichukua kuweza kwanza kuendana na malalamiko hayo lakini pia kupunguza ajali kama inavyodaiwa’ – Camillius Wambura (RPC)
.
.
‘Ilikuwa ni bahati mbaya sana wakati hao Tanroad wamefika na wakati wanaanza survey ya maeneo hayo kulitokea uhamasishaji ambao hakuwa wa lazima hakuwa wa maana kwasababu suala lilikuwa ni wa matuta uhamasishaji huo ulisababisha vurugu na kuanzia kurusha mwe na kundi kubwa lilitoka katika pande mbili za barabara kuanza kurusha mawe’- Camillius Wambura (RPC)
.
.
‘Jeshi la polisi kwa askari waliokuwepo walijaribu kuwatawala wale watu hayo pasipo kuleta madhara kwasababu tunajitahidi kupunguza madhara kwa kilengo cha hali ya juu kwa hiyob waliwatala pasipo kuleta madhara lakini kundi hilo hilo lilikuwa kubwa wakaweza kukivunja kituo kidogo cha polisi kilichopo hapa Bunju A na kukiteketeza kwa moto hapa ndani kulikuwa na maabusu watatu ambao ilibidi askari wawafungulie na kuwaamisha ili kuokoa maisha yao’- Camillius Wambura (RPC)
.
.
‘Kwa hiyo waliofanya kitendo hiki hatutawacha waendele kuchoma vituo vingine na nyumbani nyingine tutahakikisha tunawakamata wote kila mmoja na tutahakikisha tunawafikisha mbele ya vyombo vya dola mchezo huu ni uhuni lakini mchezo huu ni uhalifu hiki ni kituo kilichojengwa na wananchi wenyewe ni kituo kilichokuwa kinawahudumia wao wenyewe’ – Camillius Wambura (RPC)
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.