Wanafunzi wakiwa nje baada ya mabweni yao kuungua.
Wanafunzi wamegoma kulala mabwenini, naibu waziri atoa ushauri
MBEYA: Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Iyunga wamesababisha shule yao kufungwa kutokana na kuogopa kulala kwenye mabweni yaliyobakia wakidai wakiingia wanaona maruweruwe baada ya mengine kuteketea kwa moto hivi karibuni.

Wanafunzi hao waliliambia gazeti hili hivi karibuni kuwa kila wanapoingia katika mabweni ambayo hayakuungua wanaona maruweruwe na wakaamua kulala nje kwa siku zote tangu bweni lao lilipoungua na kuteketeza baadhi ya vitu vyao, hali iliyolazimisha uongozi wa shule kuifunga.
Wanafunzi hao wakiwa hawajui la kufanya baada ya mabweni yao kuungua.
Kufungwa kwa shule hiyo kumefanyika mapema kwani kwa kawaida ilitakiwa ifungwe karibu na Sikukuu ya Pasaka lakini sasa imefungwa Machi 11 na itaendelea kufungwa hadi Aprili Mosi mwaka huu.
Mkuu wa shule hiyo, Edward Mwantimwa alithibitisha kufungwa kwa shule hiyo kwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Tamisemi) Seleman Jaffo aliyetembelea shuleni hapo kujionea uharibifu uliotokana na moto uliounguza mabweni matatu kwa nyakati tofauti na kusababisha taharuki kubwa kwa wanafunzi.

Mwalimu Mwantimwa alisema: “Mara ya kwanza mabweni ya Nyerere na Mkwawa yaliungua Februari 29 na Machi 7, mwaka huu la Shaaban Robert nalo likaungua, jambo ambalo lilisababisha hofu kwa walimu na wanafunzi, hivyo kuyasusa mabweni mengine.”
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Tamisemi) Seleman Jaffo .
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyirembe Munasa kwa niaba ya mkuu wa mkoa alimuambia Naibu Waziri Jaffo kuwa tayari serikali ya mkoa imechukua hatua ikiwemo ya kutoa misaada na kwamba wameandaa harambee itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuchangia ukarabati wa shule hiyo.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Jaffo aliliita tukio hilo kuwa ni janga na akaahidi kuwashirikisha wabunge wote kuchangia kurudisha hadhi ya shule hiyo.
Kiongozi huyo alimtaka Mkuu wa Wilaya, Nyirembe kusimamia ukarabati wa shule hiyo na uwe umekamilika ifikapo Aprili mwaka huu.
“Kuungua kwa shule hii kumeonesha mengi yakiwamo ya uchakavu wa miundombinu,” alisema naibu waziri huyo
“Kuungua kwa shule hii kumeonesha mengi yakiwamo ya uchakavu wa miundombinu,” alisema naibu waziri huyo