Mpaka sasa video hii imetazamwa zaidi ya mara laki moja na elfu 30 kwenye mtandao wa Youtube toka ianze kuonyeshwa April 29 2014 ikiwa ni video ya kipekee na ya kiwango kingine cha juu tofauti na ilivyozoeleka kwa Sauti Sol.
Mtandao wa Kenya ghafla.co.ke umeripoti kwamba imefahamika video hii imezuiwa kuchezwa kwenye TV stations mbalimbali za Kenya kwa sababu imevunja maadili.
Kwenye Mdundo Awards jana usiku Bien Aime wa Sauti Sol alisema mwanasheria wao anashughulikia ishu ya kufungiwa kwa video yao ambayo imeambiwa inachochea ngono kutokana na uwazi wa wanaookenana ndani yake.
Hii itakua video nyingine iliyochukua headlines zinazofanana na ile ya P Unit ‘you guy’ ambayo ilifungiwa na CITIZEN TV kwa sababu ya mrembo alieliachia umbo lake kwa sana