Wednesday, December 31, 2014

NICK MINAJ AWEKA WAZI SABABU ZA KUTOA UJAUZITO AKIWA NA UMRI WA MIAKA 16

minajHitmaker wa ‘Anaconda‘ Nick Minaj ameamua kuweka wazi sababu ya kuamua kutoa mimba wakati akiwa binti wa miaka 16 na kusema maamuzi hayo yaliuvunja moyo wake.
Nilijua ningekufa baada ya kufanya vile“…Wakati huo nilikua bado binti mdogo,nilikua na wakati mgumu sana ambao sijawahi kukutana nao tena,”anasema Nick Minaj alipokua akizungumza na jarida la Rolling stone.
Kwa mujinu wa jarida hilo liliandika kuwa mtu aliyempa mimba alikua ni mzee ambaye alikua na mahusiano naye wakati bado akisoma katika chuo cha mafunzo ya muziki na sanaa cha Manhattan’s Fiorello H. LaGuardia High School of Music & Art.
“Sikua tayari kubeba ujauzito kwa wakati huo na haikua chaguo langu kwani sikuwa na chochote cha kumpa mwanangu…najua wengi hawatapenda hiki ninachoongea,”alisema.