Monday, June 1, 2015

BETHIDEI YA JACK DUSTAN KUFURU!

Imelda mtema
Mrembo aliyepata jina kupitia Shindano la Maisha Plus, Season Two, Jacqueline Dustan amefanya kufuru kwenye pati yake ya kuzaliwa (bethidei) iliyofanyika kwenye Hoteli ya Peacock jijini Dar, wikiendi iliyopita.
Jacqueline Dustan akiwa katika pozi.
Sherehe hiyo iliyokuwa na vyakula na vinywaji vya kufa mtu, ilihudhuriwa na ‘mashosti’ mbalimbali wa Jack huku ikiendeshwa na mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’ aliyeongozana na Mwigizaji Husna Idd ‘Sajent’.
Jacqueline Dustan akiwa na mwandishi wa Global publishers Imelda mtema.
Pati hiyo ilitumbuizwa na bendi ya hoteli hiyo na kilichoifanya ionekane ya kufuru ni pale Jack alipompa shilingi 20,000 kila mgeni mwalikwa kwa ajili ya usafiri wa kurudi nyumbani jambo ambalo halijawahi kufanywa na staa yeyote.