Monday, June 1, 2015

STEVE NYERERE, DUDE WAFIKA PABAYA!

Gladness Mallya na Gabriel Ng’osha
Hali mbaya! Lile bifu la waigizaji wa filamu za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na Kulwa Kikumba ‘Dude’ limefika pabaya ambapo wamekuwa wakitoleana maneno makali kwamba mmoja wao akifa hawatazikana.
Stive Nyerere.
Chanzo cha wasanii hao kugombana kilitokana na kaburi la marehemu Adam Kuambiana ambalo limejengwa hivi karibuni ambapo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Steve Nyerere aliandika waraka mrefu akiwashutumu Dude na William Mtitu kwamba wao ndiyo wanaomchafua.
Kulwa Kikumba ‘Dude’
Akieleza hali ilivyo kwa sasa, Dude alikuwa na haya ya kusema: “Unajua kusema kwangu ukweli ndiyo unanigombanisha na Bongo Muvi. Pamoja na jitihada za kupatanishwa, Steve amekataa na amesesema hata nikifa hawezi kuja kunizika.”
Kwa upande wa Steve naye alisema: “Huyo Dude aendelee na maisha yake.”