Aliyekuwa mgombea Urais wa Zanzibar na katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewashangaa viongozi wa CCM visiwani humo kwa kile alichokiita wanatafuta kura kwa udi na uvumba kama Ngedere msituni.
Seif ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa, kamwe Wazanzibar hawatasahau dhulma na chuki dhidi yao walizofanyiwa mwaka huu, hata kama Dr Shein atatangazwa na kuapishwa.
“Kinachofanyika si uchaguzi, bali ni kumtangaza Dk. Shein kuwa rais…CCM wanasaka kura utafikiri wanasaka ngedere porini…watumishi wote waliopo nje ya Zanzibar wamelazimishwa kurudi wapige kura.
“Sasa tunasubiri tu Rais atangazwe na kuapishwa. Hata wakimtangaza Dk. Shein mshindi atakuwa ni Rais wa Jecha (Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha) na CCM.
“Ukweli ni kwamba Wazanzibari wanajua rais wa mioyo yao, ni Maalim Seif na hawawezi kufuta hilo,”alisema