Sunday, May 29, 2016

Samatta Aipeleka Genk Europa League

Samatta-ushindi

Leo May 29, Mbwana Samatta ameandika historia mpya kwenye maisha yake baada ya kuisaidia timu yake ya Genk kushinda mchezo wa fainali ya play off na hatimaye kufu kucheza michuano ya Ulaya (Europa League).

Samatta ambaye alianza kwenye kikosi cha kwanza cha Genk ameisaidia klabu yake kupata ushindi wa magoli 5-1 kwenye uwanja wao wa  nyumbani (Cristal Arena) dhidi ya Sporting Charleroi.

Katika ushindi huo wa magoli 5-1, Samatta amefunga goli moja ambalo lilikuwa ni goli la pili kwenye mchezo huo. Nikolaos Karelis ambaye amfunga hat-trick kwenye mchezo huo alianza kuifungia Genk goli la kwanza kwa mkwaju wa penati dakika ya 17 kisha Samatta akazamisha bao la pili dakika ya 27 kabla ya Sandy Walsh kupiga bao la tatu dakika ya 45 na kuipeleka Genk mapumziko ikiwa mbele kwa magoli 3-1.